Saturday, August 24

Maguli ajiengua KMC, ajiweka sokoni

0


NA WINFRIDA MTOI

MSHAMBULIAJI wa KMC, Elias Maguli, ameachana na
kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa madai ya kutokuwa na
maelewano na benchi la ufundi kwa muda mrefu.

Maguli ajiunga na KMC katika dirisha dogo la Ligi
Kuu Tanzania Bara lililofanyika Novemba hadi Desemba mwaka jana.

Hata hivyo, Maguli hakuwa anapangwa mara kwa mara
katika kikosi cha kwanza kwa madai ya kuwa majeruhi.

Akizungumza na BINGWA jana, Maguli alisema baada ya
kukaa nje kwa muda mrefu katika kikosi hicho, ameandika barua ya kuachana na
klabu hiyo.

Maguli alisema kuna changamoto nyingi zilizomfanya
aachane na kikosi hicho, lakini kikubwa ni kutoelewana na uongozi wa benchi la
ufundi.

 “Watu wengi
wanafahamu mimi ni majeruhi lakini si kweli, nimeona niandike barua ya kuachana
na timu na uongozi wa KMC umekubali.

“Nimepata ofa katika timu nyingine, lakini natulia
kwanza nikisubiri ligi imalizike na kuchagua wapi na sehemu sahihi kwa mimi
kucheza,” alisema Maguli.

Share.

About Author

Leave A Reply