Tuesday, August 20

Ligi ya vijana ngazi ya Taifa kuanza Juni

0


NA MWANDISHI WETU

SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF), limesema Ligi ya Vijana Ngazi ya Taifa chini ya umri wa
miaka 15 na 17 itaanza Juni mwaka huu.

Kwa mujibu
wa taarifa iliyotumwa jana kwenye vyombo vya habari na Ofisa Habari na
Mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo, kwa sasa ligi  hiyo inaendelea ngazi ya wilaya.

Taarifa hiyo ilisema  imeanzisha kwa juhudi za  TFF katika harakati za kuendelea kuwekeza katika
soka la vijana.

Ilisema ligi ya vijana ngazi ya wilaya
inatarajia kumalizika mwishoni mwa Aprili, baadaye kuendelea ngazi ya mkoa Mei,
mwaka huu.

Taarifa hiyo ilisema TFF inaendelea
kuwekeza katika soka la vijana ambako ni msingi wa maendeleo ya soka.

Share.

About Author

Leave A Reply