Monday, June 17

Leo ni zamu ya Guinea na Cameroon, Morocco na Senegal, Azam Complex Chamazi

0


Lulu Ringo, Dar es Salaam

Baada ya ufunguzi wa mashindano ya Afcon U-17 kuanza kwa mafanikio jana kwa timu ya Nigeria na Angola kwa ushindi kwenye kundi lao A ambapo Nigeria amemfunga Tanzania 4-1 na Angola amemfunga Uganda 1-0, mashindano hayo yanaendelea leo kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini hapa.

Mechi za leo za kundi B mchezo wa awali majira ya saa kumi itazikutanisha timu za taifa la Guinea itapambana na Cameroon na mchezo wa pili utakaopigwa saa moja usiku utawakutanisha Morocco na Senegal.

Mechi hizo zinasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki lukuki kutokana na historia ya nchi hizo katika soka la ushindani.

Baada ya michezo hiyo ya leo, michezo mingina kwa timu hizi itapigwa Aprili 18 ambapo Cameroon atapambana na Morocco na Senegal atapambana na Guinea, katika Uwanaj huo wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.

Share.

About Author

Leave A Reply