Sunday, August 25

Kocha Ruvu Shooting haamini kilichomtokea

0


ZAINAB IDDY

KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting, Abdulmutik Haji, alisema
kuwa hadi sasa bado hajaamini kama kikosi chake kimesalia katika Ligi Kuu
Tanzania Bara kutokana na hali mbaya waliyokuwa nayo.

Ruvu Shooting imefanikiwa kusalia katika ligi
hiyo baada ya kumaliza ikiwa nafasi
ya 15 kwa kuvuna pointi 45, sawa na Mbao FC iliyopo nyuma yake.

Akizungumza na BINGWA, Haji alisema kutokana na
changamoto alizokutana nazo ndani ya msimu mzima,  alikuwa 
amekata tamaa, lakini mechi ya mwisho ikawaokoa.

 “Ni ngumu
kuamini, ila mwisho wa siku namshukuru Mungu kwa kutupigania na kutupa nafasi
nyingine ya kushiriki Ligi Kuu msimu ujao, tutapambana ili tusipate matatizo
kama yaliyotukumba.

“Changamoto zilichangiwa na jinsi ligi ilivyoendeshwa,
kwani hakukuwa na usawa, waamuzi nao hawakuwa sawa, miundombinu na kutuweka
katika hali mbaya kwenye msimamo.”

Share.

About Author

Leave A Reply