Tuesday, August 20

Kocha Mbeya Kwanza atamba kuiparua Majimaji

0


NA GLORY MLAY

KOCHA wa Mbeya
Kwanza, Michael Kasekenya, ametamba kuibuka na ushindi dhidi ya Majimaji katika
mchezo wa marudiano wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), utakaochezwa keshokutwa
kwenye Uwanja wa Majimaji, mjini Songea.

Akizungumza na
BINGWA jana, Kasekenya alisema atahakikisha pointi tatu zinabaki nyumbani.

Kasekenya alisema
wamejipanga vyema kuhakikisha wanapata pointi sita katika michezo miwili
iliyosalia, ikiwamo wa keshokutwa dhidi ya Mbeya Kwanza.

Alisema wachezaji
wake wapo fiti kwa mchezo huo, kwani hana majeruhi yeyote na ana imani watapata
matokeo wanayotarajia.

“Mechi zilizosalia
ni ngumu kwa kuwa zitatoa tathmini ya timu ya kupanda daraja, hivyo tunahitaji
kupata pointi sita katika michezo miwili, tunapambana na kila mchezaji anajua
lengo letu ni lipi,” alisema Kasekenya.

Hata hivyo,
aliongeza kuwa ni muhimu mashabiki kwenda uwanjani kuwapa sapoti na hamasa
wachezaji ili wafanye vizuri.

Mbeya Kwanza
wanashika nafasi ya pili katika masimamo wa Kundi B kutokana na pointi 35,
baada ya kucheza michezo 20, wakishinda michezo tisa, sare nane na kufungwa
mitatu.

Share.

About Author

Leave A Reply