Thursday, August 22

KOCHA DR CONGO AWATAJA SAMATTA, MSUVA – Bingwa

0


AYOUB HINJO NA EZEKIEL TENDWA

KOCHA wa timu ya Taifa ya DR Congo, Ibenge Florent, amewataja washambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, Simon Msuva na Thomas Ulimwengu, kuwa anawahofia katika mchezo wa leo wa kirafiki utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Taifa Stars watawakaribisha DR Congo, baada ya kutoka kupokea kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Algeria katika mchezo wa kirafiki uliochezwa wiki iliyopita.

Akizungumza jana, Florent, alisema mchezo huo utakuwa mgumu hasa kutokana na kuwa na wachezaji mahiri  kama Samatta, Msuva  na Ulimwengu, ambaye hayumo kwenye kikosi cha Taifa Stars.

“Utakuwa mchezo mgumu kwa kuwa  Taifa Stars ni moja ya timu ngumu ninazozifahamu. Ina wachezaji wenye uwezo mkubwa kama Samatta, Msuva na Ulimwengu.

“Walifungwa mchezo uliopita lakini wapo nyumbani kesho (leo), watahitaji kupata matokeo mazuri ili kuwapa furaha mashabiki wao watakaoingia uwanjani,” alisema.

Florent alisema wao wamejiandaa vizuri na mchezo huo na wachezaji wake wapo  fiti.

Kiingilio cha mchezo kitakuwa ni Sh 5, 000 kwa VIP A, B na C, wakati viti vya mzunguko kitakuwa Sh 1,000.

The post KOCHA DR CONGO AWATAJA SAMATTA, MSUVA appeared first on Bingwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.