Saturday, August 24

Kocha Baobab Queens ataka kikosi kipana

0


NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

KOCHA wa timu ya Baobab Queens ya jijini hapa, Musa
Furtune, amesema anahitaji kusajili kikosi kipana kwa ajili ya msimu ujao wa
Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake Tanzania Bara.

Baobab Queens imemaliza  nafasi ya nane katika msimamo wa ligi hiyo,
kutokana na pointi 21 huku JKT Queens ikifanikiwa kutetea ubingwa kwa pointi
66.

Akizungumza na BINGWA juzi, Furtune alisema licha ya
kikosi chake kucheza kwa kujituma, lakini kilikuwa na mapungufu.

 “Ukiwa na kikosi
kipana, mwalimu anakuwa na uwezo wa kuamua ampange nani,  ushauri wangu msimu ujao uongozi usajili
wachezaji wengi, lakini wenye uwezo,” alisema Furtune.

Kocha huyo alisema ligi ya msimu huu ilikuwa ni zuri,
licha ya changamoto ya ukosefu wa fedha iliyofanya timu nyingi zishindwe
kucheza vizuri.

“Hata sisi hatukuwa vizuri, wakati mwingine tulikuwa
tunafika kwenye mechi siku ya hiyo hiyo wachezaji wakiwa wamechoka,” alisema.

Share.

About Author

Leave A Reply