Wednesday, June 19

KELVIN JOHN ; Kinda Serengeti Boys aliyetamani kuwa tabibu wa akina mama

0


NA GROLY MLAY

LICHA ya timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’ kufanya vibaya katika michuano ya Kombe la Vijana Afrika (U-17 Afcon), mshambuliaji wa kikosi hicho, Kelvin John, ndiye aliyeonekana kivutio kutokana na uwezo wake wa kusakata kabumbu.

Kutokana
na kiwango alichoonyesha katika michuano hiyo, kilimfanya Kocha wa Taifa Stars,
Emmanuel Amunike, kumwiita katika kikosi cha awali cha kujiandaa na michuano ya
Kombe la Mataifa Afrika (Afcon2019), itayoanza Juni 21, mwaka huu, nchini Misri.

Licha
ya juzi mshambuliaji huyo kuchujwa katika kikosi cha Taifa Stars kinachoendelea
na mazoezi nchini Misri, lakini anaonekana ni hazina kubwa kwa baadaye.

Kipaji
cha mshambuliaji kilianza kuonekana wakiwa katika Kituo cha Elimu Sports
Academy kilichopo Morogoro kabla ya kushiriki michuano ya Shule za Msingi
Tanzania (Ummitashumta).

Baadaye
alichaguliwa kujiunga na Kituo cha Football House Academy cha jijini Mwanza
ambacho kimempa mafanikio makubwa.

 Je, uliwahi kujiuliza kama si soka, John
angekuwa anafanya kazi gani?

Akizungumza
na BINGWA jana, John alisema kama si soka, angependa kufanya kazi ya utabibu wa
magonjwa ya wanawake.

“Ningekuwa
daktari wa wanawake maana wanahitaji huduma nzuri, kwani wao ndio watunzaji
familia, hasa watoto, hivyo nisindependa kuona mwanamke yeyote anakosa huduma,”
anasema.

Share.

About Author

Leave A Reply