Saturday, August 24

Kahata rasmi ataja kutua Simba

0


NA WINFRIDA MTOI KIUNGO

mshambuliaji wa Gor Mahia, Francis Kahata, ameweka wazi kuwa mkataba wake na kikosi hicho unamalizika mwezi ujao na kuitaja Simba moja ya timu anayoweza kutua.

Mchezaji huyo alianza kufukuziwa na Simba hata kabla ya Meddie Kagere, lakini kilichokuwa kinambana nyota huyo ni mkataba wa Gor Mahia waliokuwa wanahitaji dau kubwa kuvunja.

Jana katika ukurasa wake wa ‘Facebook’, Kahata, aliandika kuwa mkataba wake na kikosi hicho unaelekea ukingoni, imefikia hatua ya kutafuta changamoto sehemu nyingine. 

“Mkataba wangu unafikia ukingoni Juni, mwaka huu, nimetwaa mataji matatu nikiwa na Gor Mahia, ni muda sasa wa kupata changamoto mpya.

“Uongozi wa Gor Mahia bado haujazungumza na mimi juu ya kuongeza  mkataba mpya, nafikiri nitakuwa huru kujiunga na klabu yoyote. “Ni kweli wiki iliyopita Simba walizungumza na mimi, lakini hii haina maana kuwa siwezi kuendelea kuwepo Gor Mahia, naweza kusaini mkataba mpya, sijui,” alielezea Kahata.

Tetesi zilizopo ni kwamba, si Kahata pekee anayetakiwa na Simba kutoka Gor Mahia, wapo wachezaji wengine ambao wanaendelea kufanya nao mazungumzo. Jaques Tuyisenge, ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa gumzo kwa sasa na inasemekana Simba wameshakamilisha kila kitu, ili kumng’oa mchezaji huyo ambaye ndiye aliyekuwa akimtengenezea Kagere nafasi za kutupia mabao.

Share.

About Author

Leave A Reply