Sunday, August 18

Kagera Sugar wajiandaa kuacha kilio Mwanza

0


NA GLORY MLAY

NAHODHA wa Kagera Sugar, George Kavila, amesema wataendelea
kugawa dozi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba katika
mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa Aprili 20, mwaka huu, kwenye
Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kagera Sugar ambao wanashika nafasi ya 12 katika msimamo wa
ligi hiyo, kutokana na pointi 39, wakishinda michezo tisa, wanatarajia kucheza
na Alliance keshokutwa kwenye Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza.

Akizungumza na BINGWA jana, Kavila alisema wanaelekeza nguvu
zote katika mchezo huo ili kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu dhidi ya
wapinzani wao hao.

Kavila alisema katika mchezo huo, ushindi ni muhimu kwao ili
kujihakikishia kubaki kwenye ligi hiyo.

Alisema anaamini mchezo huo utakuwa mgumu kwa kuwa wenyeji
wao hawatakubali kupoteza kirahisi ambao watacheza mbele ya mashabiki wao.

Nahodha huyo alisema kwa sasa kikosi chao kimeimarika na
wachezaji wanajua nini wanatakiwa kufanya kuhakikisha wanapata matokeo bora.

Alisema Alliance ni timu nzuri, lakini wamejipanga kuondoka
na pointi tatu, licha ya upinzani mkali utakaojitokeza katika mchezo huo.

Share.

About Author

Leave A Reply