Sunday, August 18

JKT Queens, Simba kuvaana leo SWPL

0


NA GLORY MLAY

LIGI Kuu ya Soka
ya Wanawake Tanzania Bara (SWPL), inatarajia kuendelea leo kwa timu ya JKT
Queens kuvaana na Simba Queens kwenye Uwanja wa Isamuhyo, jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia
mchezo huo, Kocha wa JKT Queens, Ally Ally, alisema wamejiandaa vizuri na hana
presha yoyote.

Ally alisema
anahitaji ushindi ili waweze kutetea ubingwa wao.

“Mchezo hautakuwa
rahisi kutokana na wapinzani wetu watahitaji pointi tatu ambazo zitawawezesha
kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hii,” alisema Ally.

Alisema
hawatadharau wapinzani wao, kwani malengo yao ni kushinda na kuendelea kuweka
rekodi katika ligi hiyo.

JKT Queens wanaongoza
katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 48, baada ya kucheza michezo 16,
wakati Simba Queens wanashika nafasi ya tatu kwa pointi 32.

Share.

About Author

Leave A Reply