Thursday, August 22

Gofu kushiriki Zone 4 Burundi

0


NA GLORY MLAY

TIMU ya Taifa ya gofu inajiandaa kushiriki michuano ya Zone
4 itakayofanyika Juni mwaka huu nchini Burundi.

Akizungumza na BINGWA jana, kocha mkuu wa timu hiyo, Hassan
Kadio, alisema wameanza maandalizi ya michuano hiyo.

Kadio alisema tayari wamechagua wachezaji katika michuano
iliyofanyika wiki iliyopita mjini Moshi   mkoani Kilimanjaro.

Alisema katika michuano hiyo, walifanikiwa kuchagua
wachezaji wanne ambao wataunda timu ya Taifa kwa ajili ya kushiriki michuano
hiyo.

Alitaja wachezaji waliochaguliwa ni Victor Joseph, Abbas
Adam, Richard Mtweve na George Sembi.

Nchi zilizothibitisha kushiriki michuano hiyo ni Kenya,
Rwanda, Ethiopia, Uganda Tanzania na wenyeji Burundi.

Share.

About Author

Leave A Reply