Friday, August 23

Four Ways mabingwa Castle Africa 5 aside

0


NA MWANDISHI WETU

TIMU Four Ways Fark FC ya Kinondoni, Dar es
Salaam, imeibuka mabingwa katika bonanza la soka  lililofanyika juzi, kwenye viwanja vya Posta
Kijitonyama.

Bonanza hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL), kupitia bia yake ya Castle Lager, ambapo mshindi alizawadiwa kikombe, medali
za dhahabu na Sh 1,500,000, katoni ya bia ya Castle Lager.

Pia mshindi wa bonanza hilo ataiwakilisha nchi
katika fainali za Caslte Africa 5s zinazotarajiwa kufanyika mwaka huu jijini
Dar es Salaam.

Four Ways Park walitwaa ubingwa huo baada ya
kupata pointi saba wakifuatiwa na Jacks Pub waliopata pointi nne na kuzawadiwa
medali za shaba, katoni ya bia ya Castle Lager na Sh 900,000.

 Mshindi
wa tatu katika fainali hizo ni Meeda Night Club FC ambao walipata pointi tatu
na kuzawadiwa medali ya fedha, katoni ya bia ya Castle Lager na Sh 600,000.

Akizungumza baada ya bonanza hilo, meneja wa Bia
ya Castle Lager, Pamela Kikuli, aliwapongeza mabingwa hao kwa kutwaa ubingwa.

Share.

About Author

Leave A Reply