Tuesday, August 20

Dybala humwambii kitu kwa Ronaldo

0


TURIN, Italia

FOWADI wa mabingwa wa Serie A, Juventus,
Paulo Dybala, anajivunia kukipiga pamoja na mfungaji wao bora msimu huu, Cristiano
Ronaldo.

Dybala alisema kuwa anapenda kucheza
pamoja na nyota mwenye uwezo kama wa Ronaldo ambaye anatambulika kwa uwezo wake
wa hali ya juu duniani pamoja na roho ya kutokata tamaa.

Curry atwaa tuzo ya Webby

NEW YORK, Marekani

NYOTA wa timu ya kikapu ya Golden State
inayoshiriki Ligi ya NBA, Stephen Curry, alikuwa ni miongoni mwa mastaa
waliotwaa tuzo za Webby mwaka huu.

Video ya ‘5 Minutes From Home’ ndio
iliyomng’arisha Curry kwenye hafla ya utoaji tuzo hizo, akiungana na nyota wa
filamu ya ‘Deadpool’, Ryan Reynolds, aliyetwaa tuzo yake kupitia kazi yake hiyo.

Khan kutundika daluga kwenye ubondia?

LONDON, England

MKALI wa ndondi nchini England, Amir
Khan, amedai ni mapema sana kuzungumzia maamuzi ya kustaafu mchezo huo licha ya
kupoteza mkanda wa WBO.

Kauli hiyo ilikuja baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Terence Crawford, wikiendi iliyopita huku akidai bado ana muda wa kufanya makubwa.

Mkongwe amvulia kofia Federer

NEW YORK,

Marekani GWIJI la tenisi, Bjorn Borg, amedai kuwa Roger Federer ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea duniani kwenye mchezo huo.

Msweden huyo mwenye umri wa miaka 62 kwa sasa, aliongeza kuwa uwezo aliouona kwa Federer kwa kiasi kikubwa umetokana na upinzani anaoupata kutoka kwa Rafa Nadal.

Wanyama awapa ‘big up’ CAF  

LONDON, England

KIUNGO na nahodha wa timu ya Taifa ya Kenya, Victor Wanyama, amelipa pongezi Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), kwa juhudi walizozionesha kuandaa michuano ya Afcon U-17 mwaka huu.

Wanyama alifurahi kuona michuano hiyo ya
vijana umri chini ya miaka 17 ikifanyika Afrika Mashariki huku Tanzania wakiwa
wenyeji wa michuano hiyo.

Palace hawana
kizuizi kwa Zaha

LONDON, England

KLABU ya Crystal Palace itaelewa
endapo staa wao, Wilfried Zaha, atatimka msimu ujao ili kupata nafasi ya
kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Beki wa timu hiyo, Scott Dann, naye
aliweka wazi kuwa Zaha anastahili kucheza michuano mikubwa kutokana na kiwango
chake kilipofikia.

Iniesta
apewa unahodha Japan

TOKYO, Japan

KIUNGO wa zamani wa Barcelona, Andres Iniesta, amepewa unahodha na klabu yake ya Vissel Kobe inayoshiriki Ligi Kuu Japan.

Iniesta mwenye umri wa miaka 34, alijiunga
na timu hiyo mwaka jana na kutoa mchango mkubwa kwenye kikosi hicho.

Share.

About Author

Leave A Reply