Sunday, August 25

CONTE ACHEKELEA MORATA KUZINDUKA – Bingwa

0


LONDON,England

KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte amefurahia hatua ya straika wake,  Alvaro Morata kuzinduka na kisha akaondokana na ukame wa mabao, baada ya juzi kufanya vyema katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Kombe la  FA  dhidi ya  Leicester City.

Katika mchezo huo, straika huyo  Morata  aliweza kuondokana na ukame ambao ulikuwa ukimuandama dakika ya  42 na kuwawezesha wanafainali  hao wa msimu uliopita kupata ushindi wa mabao  2-1  dhidi ya Leicester City katika  muda wa nyongeza.

Bao hilo lilikuwa ni la kwanza kwa mwaka huu na yalikuwa ni mafanikio yake ya kurejeshwa kwenye kikosi cha kwanza tangu apewe kisogo katika michezo mitatu iliyopita na hivyo kujizolea sifa kwa kiwango alichokionesha.

“Kwa  Alvaro ilikuwa ni muhimu sana kwake kufunga, lakini nimekunwa na kiwango chake,” Conte aliwaambia waandishi wa habari.

“Ameonesha  nidhamu  na nguvu za hali ya juu . Nadhani baoa lake ni muhimu katika siku zijazo,”aliongeza kocha huyo.

Chelsea ambao mwaka jana walichapwa na  Arsenal  watakutana na  Southampton katika hatua ya nusu fainali.

The post CONTE ACHEKELEA MORATA KUZINDUKA appeared first on Bingwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.