Monday, June 24

Chirwa ajifua kivyake Chamazi

0


NA TIMA SIKILO

MSHAMBULIAJIwa
timu ya Azam, Obrey Chirwa, ameendelea kufanya mazoezi kivyake, licha ya
wachezaji wenzake kuwa mapumzikoni.

Chirwa ambaye ni raia wa Zambia, amekuwa akifanya mazoezi
kila siku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam kwa
lengo la kujiweka fiti zaidi.

Akizungumzia mchezaji huyo, kocha msaidizi wa timu hiyo,
Idd Cheche, alisema nyota wao anatumia muda mwingi kujifua.

Cheche alisema pamoja na mchezaji huyo kumaliza mkataba
wake, lakini ameamua kufanya mazoezi binafsi ili kutunza kiwango chake.

 “Ni mchezaji makini
sana na anajua kutunza kiwango chake uwanjani, ” alisema.

Azam ilimaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu
Tanzania Bara, iliyomalizika hivi karibuni, lakini watashiriki Kombe la
Shirikisho Afrika, baada ya kutwaa ubingwa wa AzamSports Federation Cup
(ASFC).

Share.

About Author

Leave A Reply