Saturday, August 24

BATAMBUZE: CHIRWA, AJIBU HAWATAPENYA – Bingwa

0


NA JESSCA NANGAWE

BEKI wa Singida United, Shafik Batambuze, amesema itakuwa ngumu kwa washambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib, kupenya ngome yao katika mchezo wa robo fainali wa Kombe la Shirikisho la Azam, utakaochezwa keshokutwa Uwanja wa Namfua.

Akizungumza na BINGWA jana, beki huyo alisema malengo yao ni kutaka kuing’oa Yanga na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.

Batambuze alisema amejipanga vema kukabiliana na wapinzani wao ili waweze kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

“Tutahakikisha tunaing’oa Yanga ili tuweze kusonga mbele katika michuano hii. Tupo katika uwanja wetu wa nyumbani tutawabana kuanzia mwanzo hadi mwisho,” alisema Batambuze.

Katika hatua nyingine, wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi la Singida United, wamezibwa midomo kutoongea chochote kuhusiana na mchezo huo.

Nahodha wa timu hiyo, Nizar Khalfan, alisema hawezi kuongelea maandalizi ya mchezo huo bila kupata ruhusa kutoka kwa meneja wa timu hiyo, Ibrahim Mohamed.

The post BATAMBUZE: CHIRWA, AJIBU HAWATAPENYA appeared first on Bingwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.