Monday, August 26

Bares amtaja Zahera kocha bora

0


NA ZAINAB IDDY

KOCHA bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18, Abdallah Mohamed ‘Bares’, amesema kocha Mwinyi Zahera anayekinoa kikosi cha Yanga anastahili kupata tuzo.

Bares aliyeiwezesha timu ya maafande wa JKT Tanzania kubaki kwenye ligi hiyo msimu ujao, aliliambia BINGWA kuwa Zahera anastahili pongezi nyingi kwani ameisaidia timu yake kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo licha ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili.

“Timu iliyofanya vizuri katika msimu uliomalizika ni Simba na mafanikio yao yametokana na mazingira waliyoandaa, ila kwa upande wa Yanga hakuna asiyejua changamoto walizokuwa nazo lakini bado walionyesha ushindani.

“Bila shaka hali waliyokuwa nayo Yanga msimu huu kama ingekuwa ni Simba wasingeweza kupambana na huenda hata wangekosekana kwenye tano bora,” alisema Bares.

Alifafanua kwamba Yanga haikuwa vizuri kiuchumi katika msimu uliomalizika, pia hawakuwa na kikosi cha ushindani lakini Zahera alisaidia wachezaji kujituma kuanzia mwanzo wa ligi mpaka mwisho.

“Yanga imemaliza nafasi ya pili hivyo kwa upande wangu naona Zahera ana kila sifa ya kuwa kocha bora wa msimu wa 2018/19,” aliongeza Bares.

Share.

About Author

Leave A Reply