Sunday, August 25

Banda awapa tano Simba

0


NA
ZAINAB IDDY

BEKI
wa zamani wa Simba, Abdi Banda, ameipa tano timu yake hiyo ya zamani, baada ya
kusema imefanya  usajili makini na
sasa  ishindwe yenyewe kubeba  taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Banda
anayekipiga Baroka
FC ya Afrika Kusini, amekutana wachezaji wa kikosi chake hicho cha zamani
katika mazoezi jana jioni.

Simba imepiga
kambi Afrika Kusini, ikijiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi
ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na
BINGWA, Banda aliyewahi pia kuicheza Coastal Union ya Tanga, alisema anaamini
Simba itatisha na huenda ikatwaa taji la tatu kutokana na kusheheni wachezaji
mahiri.

“Wakati wanatoka
uwanja wa ndege nilikuwepo na nilionana nao lakini pia nilikwenda katika hoteli
waliyofikia(Royal Marang), nilifurahi kuonana na ndugu zangu.

“Kwa
nilivyokiangalia kikosi cha Simba , msimu ujoa utakuwa wa  furaha sana kwa mashabiki, kwa sababu
wanawachezaji wenye uwezo wa kuwapa matokeo ndani ya uwanja.

“Kama Simba
isipochukua ubingwa wa kwa mara ya tatu litakuwa ni suala la kujitakia, lakini
kwa kikosi nilichokiona wana nafasi kubwa ya kufanya hivyo,”alisema Banda.

Msimu  mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara umepangwa kuanza
Agosti 23, ambapo Wekundu hao wa tazindua kampeni zao kwa kupepetana na JKT
Tanzania.

Share.

About Author

Leave A Reply