Monday, August 19

Appiah: Nimemaliza kazi Afcon 2019

0


ACCRA, Ghana

KOCHA
wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah, amesema anakijua kwa asilimia 98
kikosi kitakachokwenda Misri kucheza fainali za Afcon 2019.

Ifahamike
kuwa ni nyota 23 pekee watakaokwea pipa kwenda kuitafutia Ghana taji la kwanza
tangu lile walilolibeba miaka 37 iliyopita.

“Napaswa
kusema najua asilimia 98 ya wachezaji (watakaokwenda Afcon),” alisema
Appiah katika mahojiano yake na kituo cha redio cha Asempa.

Kikosi
cha awali kinatarajia kutangazwa mwezi ujao kabla ya kile cha mwisho kuanikwa
Juni, mwaka huu.

Share.

About Author

Leave A Reply