Thursday, July 18

Adidas nao waingilia ishu ya Pogba, Manchester United

0


MANCHESTER, England

KAMPUNI ya kutengeneza vifaa vya michezo, Adidas,
imeiambia wazi klabu ya Manchester United kwamba isijaribu kumuuza kiungo wao, Paul
Pogba, na kama itaruhusu atue kwingineko, watalazimika kusajili mchezaji
mwingine mwenye jina kubwa.

Pogba amekuwa akifukuziwa na klabu za Real Madrid na
Juventus hivi karibuni alitangaza kwamba yupo tayari kukutana na changamoto
mpya wakati akiwa kwenye ziara ya matangazo na Barani Asia pamoja na Adidas.

Adidas, ambao wana mkataba na Pogba kuhusu masuala
ya matangazo na Pogba hawapo tayari kusikia Mfaransa huyo anaiacha Man United.

Hilo linachangiwa na hivi karibuni kampuni hiyo kusaini
mkataba mpya wa kibiashara na Red Devils hao, mkataba wenye gharama ya pauni
milioni 750.

Katika mkataba huo, Adidas wana haki ya kumtumia
mchezaji nyota zaidi wa Man Utd kutangaza bidhaa zao duniani kote, na wanahitaji
kuona klabu hiyo ikisajili supastaa mwingine kama Pogba ataondoka.

Kabla ya ujio wa Pogba mwaka 2016, Adidas walikuwa
wanamtumia Wayne Rooney kwenye matangazo yao, lakini wapo hatarini kubakiwa na mtu
mmoja tu anayefikia nguvu ya ushawishi aliyonayo Pogba, ambaye ni David de Gea.

Kwa sasa Pogba ataendelea kuwa balozi mkuu wa Adidas,
awepo Man Utd au asiwepo msimu ujao, lakini akiondoka ina maana kampuni hiyo itampoteza
‘muuza sura’ wao mkubwa ‘ndani ya klabu hiyo’.

Suala hilo linamweka kwenye presha makamu mwenyekiti
mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Ed Woodward, ambaye sasa atalazimika kutumia nguvu
ya ziada kumshawishi Pogba abaki au asajili supastaa mwingine.

Hilo la kupata mrithi wake linatarajiwa kuwa gumu kutokana
na bajeti yao ya usajili kuwa ya kawaida kufuatia mpango wao wa kufuzu Ligi ya
Mabingwa Ulaya msimu ujao kufeli.

Ili waweze kusajili wachezaji wa maana, Man United watahitaji
si chini ya pauni milioni 160 kwa klabu itakayomtaka Pogba; zikiwemo Juventus
na Madrid ambao wote wanadhaminiwa na Adidas.

Adidas watapata ahueni iwapo Pogba ataelekea kwenye
timu mojawapo kati ya hizo, lakini Man Utd watapenda abaki ili waimarishe timu
yao pamoja kabla ya msimu ujao kuanza.

Share.

About Author

Leave A Reply