Thursday, August 22

50 CENT AMKINGIA KIFUA TREY SONGZ – Bingwa

0


LOS ANGELES, Marekani

WIKI iliyopita, Trey Songz alikumbwa na kashfa ya kumtwanga ngumi mwanamke mmoja katika ‘party’ iliyofanyika Hollywood.

Songz mwenye umri wa miaka 33, aliachiwa na polisi baada ya kutoa Dola 50,000 na baadaye alitumia mitandao ya kijamii kuwashukuru mashabiki wake kwa kumuunga mkono.

Hata hivyo, staa 50 Cent ameibuka na kusema mwanamke aliyemshitaki, Andrea Buera, alidanganya ili apate mkwanja.

Kwa upande wake, Buera alimpoteza Cent na kusema ni kweli Songz alimdunda alipokutana naye kwani walishawahi kuwa wapenzi.

“Nilifika kwenye ‘party’ na ndipo Trey alipoanza kunizingua, akanipiga ngumi na kuniangusha chini,” alisema mwanamke huyo.

The post 50 CENT AMKINGIA KIFUA TREY SONGZ appeared first on Bingwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.