Sunday, August 18

Zahera: Naleta kifaa, Tuyisenge cha mtoto

0


NA HUSSEIN OMAR

KOCHA
wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema siku zote huwa habahatishi katika mambo yake,
akiwaahidi mashabiki wa timu hiyo kushusha vifaa vya nguvu kwa ajili ya msimu
ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kauli
hiyo ya Zahera imekuja baada ya kuwapo kwa tetesi kuwa timu hiyo yenye maskani
yake mtaa wa Twiga na Jangwani, imeanza mazungumzo na baadhi ya wachezaji kwa
ajili ya kuwasajili.

Akizungumza
na BINGWA jana, Zahera alisema amekiona kikosi chake kiundani, hivyo katika
usajili ujao atazingatia zaidi wachezaji wenye nguvu, roho ngumu na
wanaopambana muda wote.

“Nina
kazi kubwa sana kuhakikisha napata wachezaji ambao wana kasi, nguvu na
wanaojitoa kwa muda wote ambao wanaweza kufanya lolote kwa wakati sahihi,”
alisema Zahera.

Alisema
tayari kuna baadhi ya majina ya wachezaji ndani na nje ya nchi ambayo anayo na
wenye uwezo zaidi ya mshambuliaji wa Gor Mahia ya Kenya, Jack Tuyisenge ambaye
amehusishwa kumsajili.

“Mimi
nashangaa sana mnaandika Tuyisenge, kuna vitu vinakuja zaidi ya huyo mchezaji
wenu, muda ukifika utawaona tu wala msiwe na wasiwasi kwani nataka kuisuka
Yanga mpya ya Afrika,” alisema Zahera.

“Mimi
siwezi kuleta mchezaji mbaya hata siku moja kwa kuwa kwangu hakuna namba moja
wala mbili, siku nikiamka nitakayempanga ndiye anacheza,” alisema.

Kocha
huyo wa DR Congo alisema endapo watafanikiwa kuwanasa wachezaji hao, mashabiki
wa Yanga watakuwa wana uhakika wa kila mechi kuondoka na kicheko uwanjani.

“Timu
itakuwa bora zaidi, hawa wakishirikiana na wengine watakaobaki Yanga itakuwa
timu tishio ni kuomba Mungu atupe afya njema tufike hiyo siku,” alisema Zahera.

Alisema
baada ya kutua Yanga, aliangalia aina ya wachezaji waliokuwapo kikosini na
kuona ni vipi anaweza kuwatumia kumpa mafanikio na kusema anashukuru Mungu kwa
hilo ameweza kufanikiwa.

Alisema
pamoja na kikosi chake kutokuwa na wachezaji wa kiwango cha kutisha, lakini
amefanikiwa kuunda jeshi la nguvu kutokana na moyo wa kupambana alioupandikiza
kwa vijana wake.

Alisema
kila mchezaji aliyempa nafasi, amepambana kadiri ya uwezo wake na leo hii
kuiwezesha timu yao kuwa kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Juu
ya wachezaji ambao walikuwa wakitiliwa shaka na mashabiki, Zahera amesema kuwa
amefarijika kuona wote wameonyesha uwezo pamoja na kukabiliwa na changamoto
kadha wa kadha.

Miongoni
mwa wachezaji hao ni Klaus Kindoki, Haritier Makambo, Mrisho Ngassa na Haruna
Moshi ‘Boban’ ambao kocha huyo anaamini hawajamwangusha.

Share.

About Author

Leave A Reply