Thursday, August 22

Zahera aipotezea Azam

0


ZAITUN KIBWANA

PAMOJA
na Yanga kukabiliwa na mchezo mgumu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC,
lakini kocha wa Wanajangwani hao, Mwinyi Zahera, ameonyesha kuwapotezea
wapinzani wao kwa kuwaruhusu wachezaji wapumzike kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka
badala ya kuendelea na maandalizi ya mchezo huo.

Yanga
na Azam zinatarajiwa kuvaana Aprili 29, mwaka huu kwenye Uwanja wa  Taifa, jijini Dar es Salaam ikiwa ni mchezo wa
kwanza kwa timu hizo kukutana msimu huu.

Akizungumza
na BINGWA jana, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema Zahera ametoa mapumziko kwa
ajili ya Sikukuu ya Pasaka.

Alisema
awali kikosi hicho kilipewa mapumziko ya siku mbili, lakini Zahera ametaka
wamalize sikukuu kwanza kabla ya kurejea kwa maandalizi ya mechi dhidi ya Azam.

Hafidhi
alisema kikosi hicho kitakaporejea mazoezini hakitakuwa na mzaha kutokana na
ugumu wa mechi hiyo, huku wakiwa na lengo la kuendelea kujikita kileleni mwa
msimamo wa ligi hiyo ambapo kwa sasa wana pointi 73 baada ya kucheza mechi 31,
huku Azam wakiwa wa pili baada ya kukusanya alama 63 katika mechi zao 31.

“Leo
tulipaswa kuendelea na mazoezi lakini hatukufanya hadi Jumanne sikukuu zipite
baada ya Zahera kuongeza siku za mapumziko kutoka mbili hadi tatu na baada ya
hapo tutaendelea kama kawaida,” alisema Hafidh.

Share.

About Author

Leave A Reply