Thursday, August 22

Wawa atamani kubaki Msimbazi

0


TIMA SIKILO

BEKI wa Simba, Paschal Wawa, amesema mkataba wake unamalizika
mwishoni mwa msimu huu, lakini bado anaipa nafasi ya kwanza timu yake hiyo kabla
ya kuzifikiria nyingine ambazo zitaonyesha nia ya kumhitaji kwa msimu ujao.

Wawa aliyesajiliwa na Simba kwa mkataba wa mwaka
mmoja, amekuwa miongoni mwa mabeki waliosaidia kuifikisha timu hiyo hatua ya robo
fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika sambamba na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu
Tanzania Bara msimu huu.

Akizungumza na BINGWA hivi karibuni, Wawa, alisema
anafurahi kushuhudia akimaliza mkataba wake huku timu yake ikipata mafanikio.

Alisema endapo mabosi wa timu yake hiyo wakionyesha
nia ya kuhitaji huduma yake basi hatakuwa na pingamizi lolote.

“Kuna timu za ndani
na hata nje ambazo zinanihiji lakini kama Simba itanihitaji lazima niwape
kipaumbele kwa sababu ni timu yangu,” alisema Wawa.

Share.

About Author

Leave A Reply