Sunday, August 25

Wakali wa Goba wanaopigania fursa Ndondo Cup

0


NA ADAM MKWEPU

SOKA
ni mchezo unaopendwa duniani na wenye mashabiki wengi kuliko mingine, tena
hukusanya wadhamini wengi ambao huufanya kuwa na mvuto wa kipekee.

Katika
kila nchi, mashabiki wa soka hupenda kufuatilia ligi kuu za nchi zao na hata zile
kubwa barani Ulaya kama vile Ligi Kuu England (EPL), Ligi Kuu ya Hispania (La
Liga), Ligi Kuu ya Italia (Seria A), Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) na
nyinginezo.

Lakini
misimu ya ligi zote zinapomalizika, mashabiki wa soka hukosa burudani ya
kuburudisha nafsi zao kutokana na mahaba yao katika mchezo huo pamoja na kukosa
kuona ligi hizo, hupata fursa ya kusikia taarifa za usajili za timu zao
wanazozipenda.

Kila
shabiki wa timu fulani hupenda kusikia taarifa nzuri ya timu yake kusajili
wachezaji bora na wenye kiwango cha juu, hakuna shabiki anayependa kuona
usajili wa kuungaunga katika timu yake.

Hata
Tanzania mambo huwa ni hekaheka msimu wa usajili, wakati huo ligi zimeisha na
kila timu inajiandaa na usajili, hapa huwa hakuna ligi na wachezaji hupewa
likizo kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi.

Kwa
sasa baada ya ligi kadhaa kumalizika, Jiji la Dar es Salaam, limekuwa na mzuka
na shamrashamra za michuano ya Ndondo Cup.

Kwa
mara ya kwanza mashindano hayo yalizinduliwa rasmi mwaka 2014 na aliyekuwa
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman
Nyamlani, mashindano hayo yalifanyika kwa mara ya kwanza chini ya udhamini wake,
Dk. Mwaka, kutoka Kituo cha Foreplan Kliniki.

Hatua
ya mafanikio ya ndondo ilianza kama masihara na sasa hivi imeshika kasi,
mashabiki wa soka mara Ligi Kuu inapomalizika husubiri kwa hamu kushuhudia
Ndondo Cup, ambayo soka la ushindani huonekana kwa wachezaji wasio na majina
kuonyesha uwezo wao na hata wengine hupata fursa ya kusajiliwa na timu
zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa
hakika hamasa imekuwa kubwa katika mashindano haya ya Ndondo Cup na kufanya
makundi mengine kuona fursa za kujitangaza kupitia timu zao.

Mafundi
Ujenzi FC ni timu mpya kwenye michuano hii na imepangwa katika timu nne
kutafuta nafasi ya kufuzu hatua ya makundi.

Timu hiyo
ipo pamoja na Mwandege FC, Tandika Combine, Toroli FC zote zinagombea nafasi
moja ya kufuzu hatua ya kucheza makundi ya michuano hiyo.

Tayari
viongozi wake wameapa kufa au kupona kuhakikisha wanapata fursa ya kucheza
michuano hiyo wakiamini ni njia rahisi kuwasiliana na kutambulika na jamii.

Mhasisi wa
klabu hiyo, Jackline Mushi, anasema wanataka jamii itambue uwepo wao kutokana
na mchango wao mkubwa wanaotoa katika ujenzi.

Mkurugenzi
huyo wa Kampuni ya Ujenzi Zone Mafundi Connect, amesema licha ya kutumia
mitandao mbalimbali ya kijamii haitoshi kuwafikia jamii na kutambulika kama
hujashiriki moja kwa moja katika matukio yanayowakusanya.    

“Tunayo
foramu inayoitwa ujenzi zone mafundi connect. Ilianza kufanya kazi tangu mwaka
2012 kwenye ukarasa wetu wa fb, kule tunao wanachama 297,000.

“Kuna watu wanaojenga, wanaosambaza
bidhaa zote za ujenzi na mafundi aina zote na wadau wasiojenga pia wapo.

“Tumekuwa tukijadiliana mambo mengi
yanayohusu ujenzi wa makazi, iwapo mtu anatafuta huduma fulani huja kule
kuulizia iwe ushauri au anauza kiwanja nyumba au chochote kihusucho nyumba.

“Changamoto ya kupatikana kwa
mafundi sahihi wa fani ya ujenzi na  mwaminifu asiye mbabaishaji au
kanjanja ndiyo iliyotukutanisha,” anasema Jackline.

Mkurugenzi huyo anasema kutokana na
changamoto hizo, aliamua kuanzisha kampuni inayoitwa Ujenzi Zone Mafundi
Connect ambapo kwa sasa wanazo  taarifa
za pamoja zenye mafundi wenye fani zaidi ya 10.

“Kwenye ‘data base’ yetu kuna
mafundi wapatao 50, ingawa jumla ya mafundi tunao 500. Ikitokea mtu anahitaji
fundi anatakiwa afuate utaratibu ambapo atafika kwetu eneo la Goba na tutampa fomu ya kuunganishwa na
fundi amtakaye,” anasema Jackline.

Share.

About Author

Leave A Reply