Wednesday, August 21

Wachezaji: Yanga ingeshuka daraja

0


HUSSEIN OMAR

ZIKIWA
zimebaki siku chache kabla Ligi Kuu Tanzania Bara kufikia tamati, wachezaji wa
Yanga wamesema kama si Kocha Mkuu wao, Mwinyi Zahera, timu hiyo ingeshuka
daraja msimu huu.

Nyota
hao walitoa kauli hiyo katika hafla ya futari iliyoandaliwa na viongozi wa timu
hiyo iliyofanyika juzi katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na wadau kibao wa soka hapa nchini na Wanayanga.

Wakizungumza
na BINGWA katika tukio hilo, wachezaji Kelvin Yondani, Juma Abdul, Haruna Moshi
‘Boban’ na Amissi Tambwe, walisema Zahera si mtu wa mchezo mchezo anapohitaji
jambo lake litimie.

Beki
Juma Abdul ambaye ni nahodha msaidizi alisema Zahera ni mtu, kwani kama si
msimamo wake timu hiyo mapema ingeshuka daraja msimu huu kwa jinsi ilivyokuwa
na hali mbaya ya kiuchumi.

“Kwa
kweli kwanza tunaomba viongozi wetu wasimruhusu mwalimu Zahera aondoke, huyu
jamaa ninaamini ana kitu kikubwa zaidi cha kutufanyia hapo mwakani, kwani msimu
huu amepambana vya kutosha kuhakikisha Yanga inapata heshima yake,’’ alisema Abdul.

Kwa
upande wake, Tambwe alisema kama kuna mtu ambaye anahitaji pongezi Yanga ni
Zahera, kwani amepambana kuwajenga kisaikolojia na kuwausia kiasi kikubwa
kimawazo kuhakikisha wanapata matokeo uwanjani.

“Huyu
jamaa ni mkali sana na hana mchezo katika kazi yake hasa pale tunapokuwa
tunahitaji kushinda, kwa kweli amepambana sana kwani tulikuwa tumeshakata tamaa
kila mmoja alikuwa anawaza lake,’’ alisema Tambwe.

Naye
Yondani alisema hana kinyongo na kocha huyo licha ya kumvua kitambaa cha
unahodha na kumpa Ibrahimu Ajib, kwani hiyo yote ilitokana na msimamo wa kocha
huyo katika kuwajenga kinidhamu.

“Jamaa
noma, kwa kweli kapambana na sisi hatukutaka kumwangusha, mwakani tutafanya
vizuri zaidi kuliko mwaka huu,’’ alisisitiza Yondani.

Boban
naye hakuwa nyuma kummwagia sifa kocha huyo, akisema Zahera ni bonge la kocha,
kwani ushawishi wake ulichangia yeye kujiunga na Yanga katika kipindi cha
dirisha dogo.

“Ni
kocha mzuri, mengine tuombe uzima, mwakani tutajitahidi kufanya vizuri na
kuchukua ubingwa,’’ alisema Boban.

Share.

About Author

Leave A Reply