Saturday, August 24

Tshishimbi asaini miwili Yanga

0


NA
HUSSEIN OMAR

YANGA
imemsainisha mkataba wa miaka miwili kiungo wao mkabaji wa kimataifa kutoka DR
Congo, Papy Tshishimbi, baada ya ule wa awali kumalizika.

Tshishimbi,
ambaye kabla ya kutua Yanga alikuwa akiichezea Mbambane Swallows ya Swaziland,
amekuwa na mchango mkubwa tangu atue katika kikosi hicho cha Jangwani msimu wa
2017.

Chanzo
cha ndani kutoka Yanga kililiambia BINGWA kuwa Tshishimbi alisaini mkataba huo
jana, baada ya kufikia makubaliano ya kimaslahi na uongozi wa timu hiyo.

“Kimsingi
mambo ndio yameanza kama hivi kwa kuanza kuwasainisha wachezaji wa zamani ambao
wamemaliza mikataba yao na wamependekezwa na kocha Mwinyi Zahera kubaki,’’
kilisema chanzo hicho.

Kiungo
huyo na nyota wengine, Haruna Moshi ‘Boban’, Thaban Kamusoko, Mrisho Ngassa, Amissi
Tambwe, Athony Matheo, Barhuani Akilimali, Ramadhan Kabwili na Juma Mahadh, mikataba
yao inamalizika msimu huu.

Kwa
upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, alilithibitishia
BINGWA juu ya Tshishimbi kusaini mkataba wa miaka miwili na kusema kila kitu
kimekwisha na sasa kiungo huyo ni mali ya Wanajangwani.

“Tshishimbi
tumemalizana naye jana, tunaendelea kufanya mazungumzo na wengine ambao
wamemaliza mkataba baada ya jana kumaliza hilo zoezi,’’ alisema Mwakalebela.

Share.

About Author

Leave A Reply