Wednesday, August 21

Tambwe ampa tano Kagere

0






ZAINAB IDDY

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amis Tambwe, amempongeza
straika wa Simba, Meddie Kagere, kwa kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania
Bara, msimu wa 2018/19.

Tambwe amewahi kuwa mfungaji bora wa ligi hiyo
kwa misimu miwili tofauti, 2013/14, akifunga mabao 19, wakati akiwa Simba na
Yanga msimu wa 2015/16 akiibuka kinara kwa kufunga mabao 21.

Kagere amekuwa mfungaji bora msimu uliomalizika
hivi karibuni kwa kufunga mabao 23 na kufanikisha timu yake kutwaa ubingwa.

Akizungumza na BINGWA jana, Tambwe alisema  mwenendo wa Kagere tangu alipoanza kuchezea
Simba,  alionyesha matumaini ya kuvunja
rekodi yake kutokana  na kasi yake ya
kufunga.

 “Nampongeza
Kagere kwa uwezo alioonyesha na kufanikiwa kuibuka mfungaji bora, kwa juhudi yake  kama ataendelea kuwepo atakuja kuwa mfungaji
hata mara mbili.

“Ni mchezaji niliyemuona na kipaji cha pekee,
kazi anayofanya ndicho anachotakiwa kufanya straika yeyote,” alisema Tambwe.

Share.

About Author

Leave A Reply