Saturday, August 17

Simba watangaza dozi

0


NA ZAITUNI KIBWANA

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara,
Simba leo watashuka dimbani kuwavaa wenyeji wao Alliance FC katika mchezo wa
ligi hiyo utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Simba inavaana na Alliance FC ikiwa na kukumbuku
nzuri ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Wekundu hao wa Msimbazi wapo nafasi ya tatu
kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 24 ikijikusanyia pointi 60 huku
Alliance wakiwa nafasi ya 16 baada ya kucheza michezo 32 wakiwa na pointi 37.

Benchi la ufundi la timu hiyo, Simba likiongozwa
na Kocha Patrick Aussems limesema litatumia mchezo wa leo kuhakikisha wanaibuka
na ushindi ili kujitengezea mazingira ya kutetea ubingwa wao.

Aussems amesema wachezaji wake wako vizuri na
anatarajia watapata matokeo mazuri kwenye mchezo wa leo unaosubiriwa kwa hamu
na mashabiki wa timu hiyo.

Alisema wanaupa uzito mchezo huo ambao ni muhimu
kwao kushinda na kusisitiza ni lazima wapambane ili kutoruhusu ruhusu kipigo
kwa mara nyingine.

Alisema watacheza soka la kushambalia na kujaribu
kusaka bao la mapema ili kuwachanganya wapinzani wao ili baadaye waweze kuibuka
na ushindi.

“Tunafahamu kuwa tunahitaji kupata ushindi mzuri,
 tutapambana kuhakikisha tunapata matokeo
mazuri,” alisema Aussems.

Wakati Aussems akiyasema hayo, Uongozi wa timu
hiyo, umetangaza kufa au kupona jijini Mwanza kwa ajili ya kupata pointi sita
mkoani humo.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Haji Manara, amesema Alliance
wawasamehe kwani wametoka kujeruhiwa na Kagera Sugar hivyo lazima waibuke na
ushindi.

“Tumepoteza dhidi ya Kagera Sugar, haturakuwa na
cha msalia mtume leo, Alliance watusaheme tu,” alisema Manara.

Share.

About Author

Leave A Reply