Sunday, August 25

Sarri kuanza na Giroud mapema

0


LONDON, England

TIMU ya Chelsea imepanga kumwongezea mkataba
wa mwaka mmoja straika wa kikosi hicho, Olivier Giroud, ambaye alitajwa
kuondoka mwishoni mwa msimu huu kwa kukosa nafasi ya kucheza.

Lakini kocha wa kikosi hicho, Maurizio Sarri,
ameuambia uongozi wa timu hiyo ufanye haraka kumpa mkataba straika huyo ambaye
amepachika mabao 10 katika michuano ya Ligi ya Europa.

Hata hivyo, Chelsea walifungiwa na Shirikisho
la Soka Duniani, Fifa, kwa kukiuka sheria za usajili huku rufaa ya vigogo hao
wa England ikitupiliwa mbali.

Share.

About Author

Leave A Reply