Monday, August 26

Ramsey aibukia Italia fasta

0


TURIN, Italia

MAPEMA tu Aaron Ramsey alisafiri mpaka nchini Italia
kuangalia mchezo wa mwisho wa ligi hiyo kati ya Juventus na Atalanta uliomalizika
kwa sare ya bao 1-1.

Kiungo huyo raia wa Wales, atajiunga na kikosi cha Juventus
msimu ujao akiwa mchezaji huru kutokea Arsenal ambako alikaa miaka 11.

Ramsey ambaye alicheza michezo zaidi ya 350
ndani ya kikosi cha Arsenal, aliisaidia timu hiyo kushinda mataji mawili ya
Kombe la FA.

Tayari msimu wake umemalizika ndani ya
Arsenal baada ya kuumia goti huku kikosi hicho cha Unai Emery kikitarajiwa
kucheza mchezo wa fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Chelsea.

Share.

About Author

Leave A Reply