Saturday, August 24

Pepe aibeba tuzo ya Afrika kule Ufaransa

0


PARIS, Ufaransa

WINGA raia wa Ivory Coast anayeichezea Lille, Nicholas
Pepe, ameinyakua tuzo ya Mwafrika Bora kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Ufaransa ‘Ligue
1’.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, aliibuka
kidedea kwa kuwazima Whabi Khazri wa Tunisia (Saint-Etienne) na raia wa Senegal,
Ismaila Sarr (Rennes).

Pepe anakuwa mwanasoka wa tatu kutoka Ivory Coast kuipeleka
nyumbani tuzo hiyo kwa mabao 22 na asisti 12.

Share.

About Author

Leave A Reply