Wednesday, August 21

Msuva awafunda Umisseta Dar

0


MWANDISHI WETU

MCHEZAJI wa timu
ya Difaa El Jadida ya nchini Morocco, Simon Msuva, amewataka vijana wanaoshiriki
Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari (Umisseta) Mkoa wa Dar es Salaam, kuwa
na nidhamu ili waweze kufanikiwa.

Msuva aliyazungumza
hayo jana wakati wa ufunguzi wa michezo hiyo katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar
es Salaam.

Alisema jambo
kubwa wanalotakiwa kufanya katika michezo ili waweze kufanikiwa ni kuwa na
nidhamu, kuwaheshimu wazazi, walimu na wadogo zao.

Aidha, winga
huyo wa zamani wa Yanga aliwataka wanafunzi hao kuwa na bidii katika masomo yao
kwa kuwa michezo inaenda sambamba na elimu.

“Suala la
elimu nalo ni muhimu sana, ukiwa mwanamichezo mwenye elimu utafika mbali
zaidi,” aliongeza Msuva.

Michezo hiyo imeshirikisha wilaya zote tano za Mkoa wa
Dar es Salaam ambazo ni Kinondoni, Temeke, Kigamboni, Ubungo na Ilala.

Share.

About Author

Leave A Reply