Monday, August 26

Mkongwe awapa Man United beki

0


MANCHESTER, England

KIUNGO wa zamani wa Manchester
United, Darren Fletcher, ameiambia timu hiyo ifanye haraka kumsajili beki wa
kati wa Stoke City, Nathan Collins, mwenye umri wa miaka 18.

Beki huyo alichaguliwa katika kikosi bora cha
msimu katika Ligi Daraja la Kwanza, hiyo inaweza kumfanya kocha wa Manchester
United, Ole Gunnar Solskjaer, kushawishika kumsajili.

Fletcher amekuwa shabiki mkubwa wa beki huyo
ambaye anatajwa kuwaniwa na timu mbalimbali za Ligi Kuu zikiwamo Arsenal,
Manchester City na Chelsea.

Solskjaer anataka kuijenga Manchester United
kwa kusajili wachezaji chipukizi ambao wataishi kwa muda mrefu ndani ya kikosi
hicho.

Share.

About Author

Leave A Reply