Saturday, August 24

Messi afikia rekodi ya ‘babu’ La Liga

0


CATALUNYA, Hispania

LIONEL Messi amekinyakua kwa mara ya sita kiatu cha
mfungaji bora wa La Liga, tuzo inayotolewa na gazeti la Marca.

Kabla ya kufanya hivyo msimu huu, ni mshambuliaji wa
zamani wa Athletic Bilbao, Telmo Zarra, ndiye aliyekuwa ameibeba mara nyingi
(6).

Messi (31) aliibeba baada ya kuziona nyavu mara
mbili wakati Barca wakitoka sare ya mabao 2-2 na Eibar. Hivyo, jamaa
ameshazipasia nyavu mara 36.

Share.

About Author

Leave A Reply