Saturday, August 24

Mavoko akana kuomba msamaha WCB

0


NA MWANDISHI WETU

NYOTA wa Bongo Fleva, Richard Martin
‘Rich Mavoko’, amesema alishtushwa na taarifa zilizokuwa zinasambaa mtandaoni
kuwa ameomba msamaha ili arudi kufanya kazi na lebo ya Wasafi Classic Baby
(WCB).

Akizungumzia ishu hiyo, Mavoko
ambaye alijitoka WCB mwaka jana, alisema alisikia taarifa hizo za kizushi
kupitia mdogo wake lakini baada ya kufuatilia aligundua ni uongo hivyo
akapuuzia.

“Sijawahi kujaribu kuomba msamaha na
hakiwezi kutokea kitu kama hicho, bora nivae shati lililochanika kuliko
kutembea tumbo wazi, kikubwa naomba mashabiki zangu waendelee kunipa sapoti
kupitia wimbo wangu mpya Usizuge,” alisema Mavoko.

Share.

About Author

Leave A Reply