Thursday, August 22

Lwandamina akalia kuti kavu Zesco

0


NA MWANDISHI WETU

KOCHA Mkuu wa zamani wa Yanga, b, amekalia kuti kavu
ndani ya klabu yake ya Zesco kufuatia matokeo yasiyoridhisha katika Ligi Kuu ya
Zambia (ZSL).

Hali mbaya kwa kocha huyo wa zamani wa Yanga,
Lwandamina, imekuja baada ya kushindwa kufanya vizuri katika mechi sita za
ligi.

Zesco katika mechi hizo ilikubali kichapo cha bao
4-1 dhidi ya Zanaco, sare ya 1-1 dhidi ya Kabwe Worriors, kichapo cha bao1-0
dhidi ya Mufurila Wonderers, ilikubali sare ya 2-2 dhidi ya Lusaka Dynamos
kabla ya kutandikwa bao 1-0 na Choma Eagles.

Habari kutoka Zambia zinasema kuwa siku za kocha
huyo aliyeiacha Yanga kwenye mataa mwaka jana mwezi kama huu zinahesabika, huku
shinikizo kubwa la kuondoka kocha huyo likitoka kwa mashabiki wenye hasira.

Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na kiongozi wa
mashabiki hao, Elius Kangwa kwa uongozi wao, mbali na kueleza kuhuzunika na
matokeo hayo mabaya, iliueleza wazi uongozi huo umefeli kuendesha timu yao.

“Zesco inahitaji watu wapya, wanaoelewa mpira wa
miguu na watakaokua tayari kufanya maamuzi ya haraka kuepuka usumbufu kama huu
tunaoupata sasa, tunamwomba Ofisa Mtendaji Mkuu wetu akae mbali na timu na
asihusike na maamuzi yoyote tena hata kuajiri kocha mwingine.

“Wachezaji wote wenye umri mkubwa na waliochoka
waondoke tubaki na wachanga, kwani ni heri kupoteza mpira ukiwa na damu changa
utakuwa unajenga timu kuliko wazee.

“Ni wazi kwamba benchi la ufundi likiongozwa na
Lwandamina limeshindwa kazi, waondolewe kama tunataka kuona Zesco mpya,
tunasisitiza waturudishie Zesco yetu ya zamani,” alieleza Kangwa katika andiko
lake kwa uongozi.

Hata hivyo, uongozi wa Zesco umepanga kukutana na
mashabiki hao wenye hasira Jumamosi hii kuweza kuzungumza.

Share.

About Author

Leave A Reply