Saturday, August 24

Kocha Sevilla akiri Simba kiboko, wamtaja Niyonzima

0


THERESIA GASPER

KOCHA
Mkuu wa Sevilla ya Hispania, Joaquin Caparos, amekisifia kikosi cha Simba
kutokana na kiwango walichokionyesha katika mchezo wa kirafiki uliochezwa juzi
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika
mchezo huo wa kusisimua, Sevilla walishinda mabao 5-4, ikiwa ni baada ya kuwa
nyuma kwa mabao 3-1 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Akizungumza
baada ya mchezo huo, Caparos alisema kipindi cha kwanza Simba walicheza vizuri
na kufunga mabao matatu, lakini mabadiliko aliyofanya yalimsaidia na kupata
ushindi.

“Awali,
tuliona mchezo ni rahisi, lakini tumecheza na timu ambayo ni nzuri, inapambana.
Wamecheza mpira mzuri, kweli timu hii ni bingwa,” alisema.

Alisema
Simba ina wachezaji wazuri ambao wapo imara, ambao walipambana kwa dakika zote
90 na kupata mabao manne.

Caparos
alisema wamefurahi kucheza na timu kama ya Simba, kwani wamewapa burudani
mashabiki waliojitokeza uwanjani kushuhudia mchezo huo.

Kwa
upande wake, winga wa Sevilla, Quincy Promes, amewavulia kofia nyota wa Simba, Haruna
Niyonzima, Meddie Kagere na John Bocco kwa kiwango kizuri walichokionyesha
kwenye mchezo huo.

 “Awali nilikuwa siifahamu timu hii na wala
sijawahi hata kuisikia, lakini tumekuja na tumecheza nao tumeona walivyocheza
vizuri. Kuna wachezaji wazuri…yule aliyevaa jezi namba nane na 22 na 14, walicheza
soka la kuvutia,” alisema

Share.

About Author

Leave A Reply