Saturday, August 24

K-Lyn amkumbuka Mengi

0


NA MWANDISHI WETU

KATIKA
kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni za IPP,
Dk. Reginald Mengi, aliyefariki dunia Mei 2, mwaka huu huko Dubai, mke wake
ambaye ni mjasiriamali na Miss Tanzania 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi ‘K-Lyn’, amemkumbuka.

K-lyn amefunguka kwa mara ya kwanza
juzi toka afiwe na mumewe kupitia ukurasa wake wa Twitter, kwa kumtakia heri ya
kumbukizi ya kuzaliwa na kueleza vile yeye na watoto wao walivyomkumbuka na
walivyobaki wapweke.

“Leo
tungekuwa tunakusherehekea wewe, kama nikifumba macho yangu naweza kuona namna
unavyotabasamu pale tunapokuimbia heri ya kuzaliwa. Hakuna neno la kuelezea ni
kiasi gani mimi na watoto tulivyokukumbuka, kuamka kila siku bila wewe. Heri ya
kuzaliwa mpenzi wangu wa kweli, milele mioyoni mwetu,” alisema K-Lyn.

Share.

About Author

Leave A Reply