Wednesday, August 21

Huyo Sanchez hataki mchezo kabisa

0


MANCHESTER, England

TAARIFA zinasema kuwa
winga wa Manchester United, Alexis Sanchez, amepanga kupunguza likizo yake
kisha kurudi haraka kujiandaa na msimu mpya.

Tangu ajiunge na kikosi
hicho akitokea Arsenal, ameshindwa kuonyesha kiwango alichotarajiwa na wengi
lakini nyota huyo wa Chile anaamini muda wa kufanya hivyo umefika.

Kwa sasa Sanchez amerudi
kwao Chile kwa ajili ya kuwaona marafiki na familia huku akisisitiza kujiweka
imara zaidi kwa ajili ya msimu ujao.

Tayari timu za Juventus
na Inter Milan zimeonyesha nia ya kuhitaji saini ya winga huyo wa zamani wa Barcelona,
Arsenal na Udinese ambaye amepewa masharti ya kupunguza mshahara wake.

“Alexis amepanga kurudi
kabla ya wengine hawajafika kambini ili kuanza mazoezi akiwa na mkufunzi wake,
kwa sasa yupo Chile lakini ataenda Hispania pia,” alisema mtu wa karibu wa staa
huyo.

Share.

About Author

Leave A Reply