Wednesday, August 21

Dude afunguka kifo cha Bongo Muvi

0


NA JEREMIA ERNEST

MKONGWE wa filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba
‘Dude’, amesema kitendo cha wasanii wa Tanzania kuiga maudhui ya sinema za nje
ndicho kimechangia kwa kiasi kikubwa soko kuyumba.

Dude ambaye kwa sasa anafanya vizuri
kupitia tamthilia yake yenye maudhui ya utapeli, Bongo Dar es Salaam ameliambia
Papaso la Burudani kuwa waongozaji wanapaswa kujua hitaji la mashabiki.

“Soko liliporomoka baada ya kuiga
kuigiza maisha ya juu, kila filamu ukiangalia mtu anaendesha Range wakati
katika maisha halisi ya hapa kwetu wanaomiliki magari hayo ni wachache,” alisema
Dude.

Share.

About Author

Leave A Reply