Thursday, August 22

Conte, Inter Milan mambo safi

0


MILAN, Italia

KOCHA wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte,
anakaribia kukubali ofa ya kuifundisha timu ya Inter Milan, taarifa hiyo
ilitolewa na kituo cha Sky Sports, nchini Italia.

Inadaiwa kuwa Inter Milan watamfukuza kocha wao,
Luciano Spalletti, mwishoni mwa msimu huu na kumtwaa Conte aliyewahi
kuifundisha kwa mafanikio Juventus.

Tangu Julai 2018, Conte alikuwa hana timu
lakini dili hilo la kuifundisha Inter Milan limetokea hivi karibuni japo
inaaminika aliwahi kusema hawezi kufundisha timu nyingine nchini humo zaidi ya
Juventus.

Share.

About Author

Leave A Reply