Thursday, August 22

Bocco aongeza mwaka Simba

0


TIMA SIKILO

HATIMAYE mshambuliaji wa Simba, John Bocco,
ameongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi Simba na hivyo kuzima tetesi za
kuhusishwa na klabu yake ya zamani ya Azam iliyokuwa imepanga kumrejesha
Chamazi, Dar es Salaam.

Habari zilizonaswa na BINGWA jana kutoka kwa mmoja
wa vigogo wa Simba, zinasema kuwa Bocco ni miongoni mwa wachezaji ambao klabu
hiyo haikuwa tayari kuwapoteza kutokana na mchango wake Msimbazi.

“Bocco tayari ameshaongeza mkataba wake wa mwaka
mmoja zaidi. Ni mchezaji aliyetoa mchango mkubwa sana Simba akiwa kama kiongozi
wa wenzake na mchezaji pia.

“Akiwa kama nahodha wa timu, ametekeleza majukumu
yake ipsavyo lakini kama mchezaji, ametoa mchango mkubwa kuiwezesha timu kufika
robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa tukiwa katika nafasi kubwa ya
kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mchezaji kama huyo huwezi kumwacha
kirahisi,” alisema kigogo huyo.

Katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Bocco
alitoa mchango mkubwa mno, akifunga mabao muhimu na kutoa pasi za mabao, huku
hadi jana akiwa amecheka na nyavu mara 15 Ligi Kuu Bara na kuchangia mengine
lukuki.

Mbali ya Bocco, kigogo huyo mwenye ushawishi wa aina
yake Simba, alisema kuwa wapo katika mchakato wa kumalizana na kiungo wao,
Jonas Mkude kabla ya kuwageukia wengineo.

Hadi sasa, Simba ipo kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania
Bara, ikiwa na pointi 88 baada ya kushuka dimbani mara 35, ikiwa imebakiza
mechi tatu tu kuhitimisha ligi hiyo inayofikia tamati mwishoni mwa wiki hii.

Share.

About Author

Leave A Reply