Tuesday, August 20

ROCHDALE YAICHOMOLEA SPURS DAKIKA YA MWISHO, SARE 2-2 FA

0


Mark Kitching wa Rochdale akiruka juu kuondosha mpira kwa kichwa kwenye boksi la penalti la timu yake hiyo ya Daraja la Kwanza katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la FA England uliomalizika kwa sare ya 2-2 leo Uwanja wa Crown Oil Arena mjini Rochdale, Greater Manchester. Mabao ya Rochdale yalifungwa na Ian Henderson dakika ya 49 na Steve Davies dakika ya 90 ma ushei, wakati ya Spurs yalifungwa na Lucas Moura dakika ya 59 na Harry Kane kwa penalti dakika ya 88. Timu hizo sasa zitarudiana Uwanja wa Wembley kutafuta nafasi ya kwenda Robo Fainali, ambako watakutana na mshindi kati ya Sheffield Wednesday au Swansea mwezi ujao PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

Read More

Share.

Comments are closed.