Sunday, April 21

NDEMLA ANAONDOKA LEO KWENDA SWEDEN KUFANYA TENA MAJARIBIO TIMU ILE ILE

0


NDEMLA ANAONDOKA LEO KWENDA SWEDEN KUFANYA TENA MAJARIBIO TIMU ILE ILE – BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINENDEMLA ANAONDOKA LEO KWENDA SWEDEN KUFANYA TENA MAJARIBIO TIMU ILE ILE – BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIUNGO chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Said Hamisi Ndemla anatarajiwa kuondoka leo mjini Dar es Salaam kwenda Sweden kwa majaribio mafupi katika klabu ya AFC  Eskilstuna ya Ligi Kuu ya nchini humo.
Ndemla mwenye umri wa miaka 22, alifuzu majaribio katika klabu hiyo Novemba mwaka juzi (2017) chini ya kocha Muingereza Michael Jolley, lakini akasaini mkataba mpya kuendelea kuichezea Simba na kuachana na ofa hiyo.
Ila sasa, Simba baada ya kupata viungo wengine bora kama Hassan Dilunga na Mzambia Clatous Chama wapo tayari kumuachia Ndemla na kijana huyo anakwenda kujaribu tena bahati yake chini ya kocha mpya, Nemanja Miljanovic.

Said Ndemla anaondoka leo Dar es Salaam kwenda Sweden kwa majaribio klabu ya AFC  Eskilstuna


Miljanovic amesema japokuwa Ndemla alifuzu majaribio Novemba mwaka 2017, lakini atahitaji kujiridhisha juu ya uwezo wake kwa majaribio mafupi tu wiki hii.
Ndemla ataondoka pamoja na mshambuliaji mwingine chipukizi wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Rashid Chambo wa JKT Ruvu jioni ya leo.
Chambo yeye atapewa wiki wiki mbili za majaribio katika klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Sweden ijulikanayo kama Allsvenskan.
Share.

Leave A Reply