Tuesday, July 23

MATA AIZINDUA MAN UNITED YATOKA NYUMA NA KUIPIGA JUVE 2-1 DAKIKA 10 ZA MWISHO

0


MATA AIZINDUA MAN UNITED YATOKA NYUMA NA KUIPIGA JUVE 2-1 DAKIKA 10 ZA MWISHO – BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINEMATA AIZINDUA MAN UNITED YATOKA NYUMA NA KUIPIGA JUVE 2-1 DAKIKA 10 ZA MWISHO – BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE

Juan Mata akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Manchester United bao la kusawazisha dakika ya 86 kwa shuti la mpira wa adhabu ikitoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya wenyeji, Juventus zikiwa zimesalia dakika 10 katika mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Allianz mjini Torino. Cristiano Ronaldo alianza kuifungia Juve dakika ya 65 akimalizia pasi ya Leonardo Bonucci na baada ya Mata kusawazisha, Alex Sandro akajifunga dakika ya 90 kuipatia Man United bao la ushindi.
Ushindi huo unafufua matumaini ya Man United kwenda 16 Bora, ikifikisha pointi saba katika mechi ya nne, nyuma ya Juventus yenye pointi tisa za mechi nne, ikifuatiwa na Valencia yenye pointi tano na Young Boys pointi moja baada ya zote kucheza mechi nne kila moja 
Share.

Leave A Reply