Wednesday, August 21

MAMA WEAH AHUHUDHURIA UZINDUZI AFCON YA WANAWAKE 2018

0


UZINDUZI wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake nchini Ghana kuanzia Novemba 17 hadi Desemba 1 mwaka 2018 umefanyika jana.
Sherehe hizo zilizofanyika mjini Accra zilizohuhudhuriwa na Balozi Soka ya Wanawake wa Shirikisho la Soka Afrika na mke wa Rais wa Liberia, Mama Clar Weah na viongozi wengine wa Serikali.
Katika hotuba yake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ndani ya Maandalizi, Freda Akosua Prempeh aliyaahidi mataifa mengine mashindano mazuri, akisema; “Tunaweka kila kitu katika nafasi yake kuhakikisha mashindano yanafanikiwa,”.

“Hii ni mara ya kwanza sisi kama nchi tunaandaa kitu kama hiki kwa mchezo wa wanawake na tunatarajia kufanya vizuri wakati wa mashindano na baada,” alisema.
Kaulimbiu ya mashindano ni; “Tunaweza kufanya hivi” na mechi zinatarajiwa kuchezwa katika miji ya Accra na Cape Coast kwenye viwanja vya Accra Sports na Cape Coast.
Washindi watatu wa juu, wataiwakilisha Afrika kwenye Fainali za Kombe la Dunia la FIFA nchini Ufaransa mwaka 2019.

Read More

Share.

Comments are closed.