Monday, August 19

IBRAHIMOVIC AHAMIA RASMI MAREKANI BAADA YA KUTEMWA MAN UNITED

0


MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic ametangaza kuwasili LA Galaxy kwa staili ya aina yake akiweka tangazo la ukurasa mzima kwenye gazeti la Times.
Mshambuliaji huyo mkongwe ameacha sehemu kubwa wazi na kuweka maneno; “Mpendwa Los Angeles, unakaribishwa”, akimalizia na saini yake chini.
Pia amepigwa picha akiwa na jezi ya Galaxy kwa mara ya kwanza, ikiongoza ukurasa wa michezo wa LA Times. 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 raia wa Sweden, Ibrahimovic amehamishia njaa yake ya mataji LA Galaxy mara tu baada ya Manchester United kukubali kumruhusu kuondoka. 

Akiwa ameondoka Old Trafford, Ibrahimovic ameposti picha katika ukurasa wake wa Instagram, akiwa amevalia kama muhubiri wa biblia huku ameshikana mikono na kuvutana na Shetani Mwekundu. Red Devil whilst dressed in biblical white robes. 

Zlatan Ibrahimovic ametangaza kuwasili LA Galaxy kwa staili ya aina yake PICHA ZADI GONGA HAPA  

REKODI YA IBRAHIMOVIC RECORD AT UNITED 

Mechi – 53
Mabao – 29
Pasi za mabao – 10
Mataji:
  • Kombe la Ligi 
  • Europa League  
Akiwa ana umri wa miaka 36, mkongwe huyo wa Sweden, Ibrahimovic anatarajia kuongeza idadi ya mataji katika kabati lake Marekani.
Ibrahimovic alikuwa tayari kujiunga na LA Galaxy mara baada ya Man United kukubali kuvunjiana naye mkataba. 
Akiwa LA Galaxy, Ibrahimovic atakuwa analipwa kiasi cha Pauni Milioni 1 kwa mwaka na amesaini mkataba wa kumalizia msimu huu. 
Mashabiki wapya wanaweza kumuona Ibrahimovic mapema tu Machi 31 akiichezea timu hiyo dhidi ya mahasimu, LAFC. 
Huo utakuwa mchezo sahihi kwake kuanza nao ili kuwakamata mashabiki kama atafunga bao dhidi ya mahasimu. 

Read More

Share.

Comments are closed.