Friday, July 19

Watu 6 Watiwa Mbaroni Kwa Tuhuma zaWizi Jijini Mwanza

0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunawashikilia wezi sita wa makosa ya kuvunja nyumba usiku na kuiba na kupatikana na vitu mbalimbali vya wizi katika operesheni kabambe inayoendelea katika kata ya Igogo Wilayani Nyamagana na maeneo mbalimbali.

Operesheni hiyo kabambe ya kipindi cha wiki moja imefanyika, baada ya kupatikana kwa taarifa toka kwa raia wema kwamba katika mitaa ya Maruru na Bugarika iliyopo kata ya Igogo Wilayani Nyamagana kipo kikundi cha wezi wanaofanya kazi ya kuvunja nyumba usiku na kuiba. Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo, kikosi maalumu cha askari wenye uweledi wa hali ya juu kilifanya operesheni kabambe katika kata hiyo na kupita chocho kwa chocho na kufanikiwa kuwakamata wezi hao sita wakiwa na vitu hivyo walivyoiba.

Wezi hao waliokamatwa katika operesheni hiyo ni;

 1.  Wilium Alex, miaka 24, dereva bodaboda, mkazi wa igogo
 2.  Peter Deogratius, miaka 22, Mkazi wa Bugarika
 3.  David Yusuph, miaka 18, dereva bodaboda, mkazi wa bugarika
 4.  Godfrey Joseph, miaka 28, mkazi wa bugarika.

Aidha watuhumiwa wawili ambao ni;

 1.  Rashid Ramadhan, miaka 32, mkazi wa maruru – Igogo na
 2.   Ester Izack, miaka 55, makazi wa maruru –Igogo, hawa wanashikiliwa kwa kosa la kupokea vitu hivyo vya wizi na kuviuza kwa watu mbalimbali.

Pia wezi hao walikamatwa na vitu vifuatavyo;

 1.     Pikipiki mbili aina ya SUN LG, ya kwanza ina namba T.758 CAG chassess namba LBRSPKB 57J9001020 na Engine namba KL1162 FMI12TG1309 na ya pili ina namba T.680 BTJ chassess namba LKIPCKL11E1043123 na Engine namba 162FMJD0003787.
 2.     Engine moja ya pikipiki aina ya Sun LG yenye namba SL162FMJ-2*18913674*
 3.     Fridge moj ya aina ya LG.
 4.     Flat screen mbili aina ya  Samsung inchi 32 na meza ya TV Moja
 5.     Laptop mbili aina ya dell na Aspires
 6.     Computer moja aina ya desk top na monitor yake.
 7.     Radio Sub wooffer moja  aina ya LG na speaker zake tano na deck yake
 8.     Radio Sub wooffer moja aina ya Greevox na speaker zake mbili
 9.     Speaker tatu za radio aina ya Seapiano
 10.     King’amuzi kimoja aina ya Continental na remote tatu
 11.     Pasi mbili aina ya zec na nippotec
 12.     Jiko la gas aina ya ORYX na mtungi wa gas aina ya ORYX.
 13.     Safuria kumi, Magodoro mawili moja aina ya Supper banco na lingine aina ya Tanform na mashuka mawili makubwa.
 14.     Radio moja aina ya Kenwood RXD.V890 yenye namba 71101776.
 15.     Mitungi miwili mikubwa ya gas aina ya ORYX.
 16.     Fridge moja na Freezer mbili.
 17.     Televisheni tatu, ya kwanza aina ya SONY Inchi 16, ya pili aina ya SAMSUNG Inchi 18 na ya tatu aina ya Star times flat screen inchi 21.
 18.     Radio Sub wooffer tatu na speaker zake sita.
 19.     Computer desk top moja na CPU yake
 20.     Majiko matatu ya gas
 21.     Mashine moja ya kupimaq presha
 22.     Nguo mbalimbali zilizofungwa kwenye mafurushi mawili.
 23.     Bidhaa mbalimbali za dukani, mzani mmoja wa dukani, chupa tupu za bia cret tano na pasi mbili
 24.     Deck aina mbalimbali sita na remote mbalimbali kumi na tano
 25.     Bomba la kutolea moshi la pikipiki, meza ndogo moja na meza ya TV.
 26.     Mashine mbili za kunyoa nywele, chupa ya chai moja kubwa na viatu pea moja.

Vilevile wezi hao pia walikamatwa na vifaa mbalimbali walivyovitumia kutendea uhalifu wa kuvunja na kuiba ambavyo ni;

 1.     Mtalimbo mmoja wa chuma
 2.     Nondo kipande kimoja kilichochongwa
 3.     Mkasi mmoja mkubwa wa kukata makufuli
 4.     Bisi bisi tatu na mapanga mawili.
Polisi tunaendelea na mahojiano na watuhumiwa wote sita, huku msako mkali ukiendelea katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza. Pindi uchunguzi ukikamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, tunatoa onyo kwa wananchi wa Jiji na Mkoa wa Mwanza hususani vijana wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kuwa waache mara moja kwani ni kosa la jinia na endapo watabainika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Sambamba na hilo tunaendelea kuwaomba wananchi waendelee kutupatia ushirikiano kwa kutupa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

 

Advertisement

==

Advertisement

Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==

….

===

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Share.

About Author

Leave A Reply